NMB leo imefungua tawi jipya katika mji maarufu wa Kibaigwa,Dodoma.
Tawi
hilo litakuwa na huduma zote za kibenki kama yalivyo matawi mengine ya
NMB nchini kote.
Tawi
la Kibaigwa limefunguliwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa Kongwa, Mh Job Ndugai.
Kufunguliwa
kwa tawi la Kibaigwa kunafuatia mahitaji ya muda mrefu ya wateja wa NMB
wa eneo hilo wa kupata tawi lenye nafasi ya kutosha .Aidha eneo hili
ni karibu
zaidi na wafanyabiashara wengi ambao ni wateja wakubwa wa NMB na
wananchi kwa ujumla .
Kwa
kutambua pia nia ya kuendelea kuchangia huduma mbali mbali za kijamii,
benki ya NMB inatoa shilingi Milioni 10 kwa ajili ya hospitali na shule
kama shukrani
za Benki kwa wananchi wa Kibaigwa kwa kuendelea kwao kuunga mkono
maendeleo ya benki.
NMB
ndiyo benki inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina
matawi zaidi ya 150, ATM Zaidi ya 500 nchi nzima pamoja na idadi ya
wateja inayofikia Milioni
mbili hazina ambayo hakuna benki yenye nayo.
NMB leo imefungua tawi jipya katika mji maarufu wa Kibaigwa,Dodoma.
Reviewed by Unknown
on
Tuesday, September 30, 2014
Rating: