Top Ad unit 728 × 90

.

Wakati Chidi Benz Yupo Chini Ya Ulinzi,Huu Ujumbe Wake Kutoka Kwa Ray C.

Wakati Rapper Chid Benz yupo chini ya ulizi kwa tuhuma za kukamatwa na dawa za kulevya kwenye uwanja wa ndege, msanii Ray C ambaye hivi karibuni aliripotiwa kupigwa vibaya na rapper huyo ameandika ujumbe huu kwa Chid Benz.

"Pole kaka yangu Chidi Benz,Naumia kuona tatizo uliokuwa nalo bado haujalitaftia jibu unalijua la kutatua tatizo lako,Mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi Pamoja,Tatizo ulilonalo na Mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu,nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu!nadhani janga hili lililokukuta litakuwa Kama jibu kwako kwamba unakoenda si salama kabisa kaka yangu ni bora ubadilishe njia ili uweze kuungana nasi kwenye tiba ya Methadone kwani ndio Kiboko ya madawa ya kulevya!!!!Kama Mimi mwanamke nimeweza najua Hata wewe utaweza!!!!Tanzania bila madawa ya kulevya Inawezekana !!Watanzania tusimyanyapae Msanii wetu kwani Uteja ni ugonjwa Kama ugonjwa mwingine na Unazuilika na Kutibika,Ana kipaji na Ana uwezo wa kurudi tena kwenye Sanaa,Tumuombee mema.........Tanzania Stand Up n Wish Him Luck............With Love,Ray C Foundation."
Sammisago.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram , Twitter Na Facebook
Wakati Chidi Benz Yupo Chini Ya Ulinzi,Huu Ujumbe Wake Kutoka Kwa Ray C. Reviewed by Unknown on Saturday, October 25, 2014 Rating: 5
All Rights Reserved by SamMisago.Com © 2014 - 2015
WebDesigned by iDodo enterprises

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.