Matapeli wanaswa wakitaka kumliza RPC wa Mwanza
Watu nane wakazi wa jijini Mwanza wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu wakitumia jina la kamanda wa polisi mkoa huo, Valentino Mlowola, kupitia namba ya simu waliyosajili.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda Mlowola, amesema watu hao wamekuwa wakiwatapeli wananchi kwa kutumia namba ya simu waliyosajili Novemba 3 mwaka huu kwa jina lake.
Mlowola alisema Novemba 4 mwaka huu, matapeli hao wakitumia namba hiyo walimpigia mtu aliye karibu naye na kudai anahitaji fedha kwa ajili ya kulipia ada ya watoto wake waliopo shuleni.
Kamanda huyo amemtaja kinara wa utapeli huo ni Evadius Grashia (30) mkazi wa Ghana wilayani Ilemela mkoani humo aliyesajili simu kwa namba 0719 910914.
Amewataja matapeli wengine walionaswa katika mtego wa polisi ni Yusuph Mwanga (28) mkazi wa Kiloleli, Hamza Hussein (36) mkazi wa Pasiansi, Goodlucky Kahumbula (42) wa Kiseke PPF, Lameck Rambati, Maiko Ngaiza (42) wa Nyasaka, Edisoni Nikolaus (42) wa Kilimahewa na Deogratius Mushukuma, na kuwatahadharisha wananchi kuepukana na utapeli wa namna hiyo hususani kipindi hiki cha kuelekea sikukuu.
Sammisago.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia Instagram , Twitter Na Facebook

Reviewed by Unknown
on
Tuesday, November 18, 2014
Rating: