Top Ad unit 728 × 90

.

Wizara ya maliasili na utalii kupitia Sheria zote za makosa dhidi ya wanayama pori,Nyalandu haridhishwi na Sheria za sasa

Wizara ya maliasili na utalii inatarajia kupitia Sheria zote za makosa dhidi ya wanayama pori kwa lengo la kufanyia maboresho Sheria za adhabu kwa watuhumiwa wa makosa ya ujangili.
Akizungumza mwishoni mwa wiki Jijini Arusha, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu katika Mkutano wa Kimataifa wa kikanda , ulioshirikisha nchi zaidi ya 9 ulimwenguni, ambao uliokuwa ukijadili
mikakati na mbinu ya kukabiliana na mauaji ya tembo na wanyama wengine, katika hifadhi mbambali kwenye nchi hizo, amesema  endapo wataondoa sheria zenye makosa na kuziboresha majangili wataogopa.

Amesema watazipitia  Sheria hizo kwa lengo la kuongeza adhabu kwa watuhumiwa wa vitendo vya ujangili, ili waogope kuendesha ujangili.

Nyalandu amesema haridhishwi na Sheria za sasa hivi kwani  adhabu zinazotolewa kwa
watuhumiwa wa ujangili ni ndogo, ila Wizara wanatarajia kupitia Sheria zote zinazohusu makosa dhidi ya wanayamapori,  kwa lengo la kuweza kuangalia namna ya kuongeza adhabu.

Amesema hadi hivi sasa silaha zaidi ya 3,000 zinazotumika katika vitendo vya ujangili, ikiwemo sihala za kivita kama vile AK 47 na Gobore,zimeweza kukamatwa na kwa kipindi cha Mwaka 2013, watuhumiwa
1816 walikamatwa na kesi zao zinaendelea katika Mahakama mbalimbali hapa nchini.
Sammisago.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia Instagram , Twitter Na Facebook 
Wizara ya maliasili na utalii kupitia Sheria zote za makosa dhidi ya wanayama pori,Nyalandu haridhishwi na Sheria za sasa Reviewed by Unknown on Monday, November 10, 2014 Rating: 5
All Rights Reserved by SamMisago.Com © 2014 - 2015
WebDesigned by iDodo enterprises

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.