Top Ad unit 728 × 90

.

Chidi Akamatwa Airport Na Dawa Za Kulevya

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Chidi Benz amekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam akiwa anaelekea Mbeya kwenye show ya Instagram Party ambayo inatarajiwa kufanyika kesho.

Chidi amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea uwanjani hapo ambapo alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.

Kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikua zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae pia kijiko na Chid Benz amekiri mwenyewe kuwa hizo dawa ni zake pamoja na hivyo vifaa
Sammisago.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram , Twitter Na Facebook
Chidi Akamatwa Airport Na Dawa Za Kulevya Reviewed by Unknown on Saturday, October 25, 2014 Rating: 5
All Rights Reserved by SamMisago.Com © 2014 - 2015
WebDesigned by iDodo enterprises

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.