Msanii Hisia ambaye aliiwakilisha vyema sana nchi yetu katika mashindano ya Tusker Project Fame mwaka jana anakaribia kuachia wimbo wake mpya uitwao GIVE ME A CALL hapo tarehe 25 Octoba katika show ya live. Katika kuusubiri wimbo huo tujikumbushe track yake ambayo imeshika chati nchini Kenya kwa wiki 6 mfululizo iitwayo MAWAZO. Wimbo huu pia unapatikana kama acapella, yaani vocal tu, ili wapenzi wake tusikie ni kwanini Hisia aliweza kufanya vizuri vile kwenye mashindano ya Tusker Project Fame.
Kwa wale wote watakao taka kufika kwenye show yake itafanyika tarehe 25/10/2014 Alliance Francaise kuanzia saa moja jioni.
Sammisago.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia >> Instagram , Twitter Na Facebook