Hii Asilimia Ya Madini Ya Tanzanite Yanayotoroshwa Nje Ya Nchi Kila Mwaka.
Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Paul Masanja, amesema hayo wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Vito, yanayofanyika jijini Arusha na kukutanisha washiriki zaidi ya 500, huku kampuni 69 zikishiriki maonyesho hayo.
Masanja ametoa mfano wa mwaka 2013 ambapo Tanzania ilipata mapato yanayofikia dola za Marekani milioni 38 kutokana na Tanzanite, wakati Kenya walipokea Tanzanite yenye thamani ya dola milioni 100, huku India ikipata dola milioni 300 za madini hayo.
Amesema kuwa kutokana na hali hiyo, serikali imeamua kujenga jengo la kuuzia madini hayo na litakapokamilika hakuna mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza madini hayo nje ya jengo hilo kama ilivyo sasa.
Sammisago.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia Instagram , Twitter Na Facebook
Hii Asilimia Ya Madini Ya Tanzanite Yanayotoroshwa Nje Ya Nchi Kila Mwaka.
Reviewed by Unknown
on
Thursday, November 20, 2014
Rating: