Hizi Takwimu Za Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI Kwa Watoto.
Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Pindi Chana wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa la VVU na UKIMWI kwa watoto linalofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo jijini Dar-es-salaam.
Dkt . Chana alisema asilimia 39 ya watoto walio katika hatari ya kupata maambukii ya UKIMWI hupimwa vipimo vya kubaini maambukizi ya VVU ndani ya miezi miwili baada ya kuzaliwa hivyo basi kuna umuhimu kwa watoto hawa kupata huduma za tiba mapema.
Akizungumzia maambukizo ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto waziri huyo alisema Tanzania imepiga hatua katika kuzuia maambukizo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto lengo likiwa ni kutokomeza kabisa maambukizi mapya kwa watoto wachanga.
Sammisago.com ndio mtandao wako kwa habari za burudani Africa na nje, Tuwe pamoja huku pia Instagram , Twitter Na Facebook
Hizi Takwimu Za Maambukizi Ya Virusi Vya UKIMWI Kwa Watoto.
Reviewed by Unknown
on
Thursday, November 20, 2014
Rating: