Serikali Yaombwa Kurekebisha Sheria Inayoruhusu Mwanafunzi Mjamzito Kufukuzwa Shuleni.
Chama cha wanahabari Wanawake Tanzania
(TAMWA) kimeitaka serikali kufanya marekebisho ya sheria inayoruhusu mwanafunzi
mjamzito kufukuzwa shuleni ili ziendane na wakati uliopo na wanafunzi wanaopata
ujauzito kupata fursa ya kuweza kuendelea na masomo na kupunguza idadi ya
wanawake tegemezi kutokana na kukosa elimu.
Akizungumza katika mahojiano na East Africa
Radio Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Valerie Msoka amesema kuwa wanafunzi
wajawazito wanafukuzwa shule kimakosa kutokana na sheria ya makosa ya jinai
kutotaja kosa la ujauzito kama kosa la kimaadili hivyo kutaka kurekebishwa kwa
sheria hiyo itakayotoa nafasi kwa mwanafunzi kujifungua na kuendelea na masomo.
Serikali Yaombwa Kurekebisha Sheria Inayoruhusu Mwanafunzi Mjamzito Kufukuzwa Shuleni.
Reviewed by Unknown
on
Thursday, November 06, 2014
Rating: