Hukumu Ya Oscar Pistorius,Miaka Mingapi Jela,Upande wa mashitaka Ulitakaje,Viko Hapa
Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius amehukumiwa kwenda jela miaka 5 baada ya kupatikana na hatia ya
kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Jaji Thokozile Masipa ametoa hukumu hio na kueleza kuwa kauli yake ya mwisho kabla ya kutoa hukumu kuwa hii ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo.
Upande wa mashtaka ulitaka mwanariadha huyo apewe kifungo cha miaka 10 gerezani baada ya kupatika na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa ndani ya nyumba yake.
Upande wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
Hukumu Ya Oscar Pistorius,Miaka Mingapi Jela,Upande wa mashitaka Ulitakaje,Viko Hapa
Reviewed by Unknown
on
Tuesday, October 21, 2014
Rating: