Msanii YP [Yessaya Ambikile] Wa TMK Wanaume Family Afariki Dunia,Haya Maneno Machache Kutoka Kwa Fella Kuhusu Msiba.
Msanii maarufu wa kundi la TMK Wanaume
Family YP [Katikati] Amefariki dunia usiku wa jana katika hospitali ya Temeke
baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kifua kwa muda mrefu.
Kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Family
Said Fella amesema "ratiba ya mazishi bado haijapangwa, kaka yake na
ndugu zake wengine wanasubiriwa na mpaka mchana leo ndio tutajua
marehemu anazikwaje"
Fella anasema marehemu alisumbuliwa na
kifua kwa muda sasa na alikuwa anatumia dawa, Alizidiwa siku chache
nyuma na kupelekwa hospitalini. Wazazi wake walifariki zamani ila
walezi wake wapo Keko na ndio msiba ulipo.
Msanii YP [Yessaya Ambikile] Wa TMK Wanaume Family Afariki Dunia,Haya Maneno Machache Kutoka Kwa Fella Kuhusu Msiba.
Reviewed by Unknown
on
Tuesday, October 21, 2014
Rating: